Idara ya uhamiaji kuchapisha pasipoti 10,000 kwa siku,asema Kindiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Idara ya uhamiaji ina uwezo kuchapisha pasipoti 10,000 kwa siku, ili kukabiliana na mahitaji ya juu ya pasipoti 5,000 kwa siku kote nchini.

Kulingana na waziri wa usalama wa kitaifa Kithure kindiki mashine mpya mbili zilizonunuliwa zina uwezo wa kuchapisha pasipoti 300 kwa lisaa kila moja.

Idadi hiyo ina maana kuwa pasipoti 4,800 zitachapishwa kwa muda wa saa nane, kinyume na sasa ambapo mashine iliyopo ina uwezo wa kuchpisha pasipoti 1,000 kwa saa nane.

Share This Article