Idara ya polisi yawasambazia chakula waathiriwa wa mafuriko

Martin Mwanje
1 Min Read

Ilikuwa na afueni kwa waathiriwa wa mafuriko katika maeneo mbalimbali ya nchi baada ya Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS kuwasambazia chakula na bidhaa zingine za matumizi leo Alhamisi. 

Miongoni mwa bidhaa zilizosambazwa na NPS ni maziwa na maji.

Serikali imetangaza kuwa jumla ya kaunti 38 kati ya 37 zimekumbwa na mafuriko ambayo yameainishwa kuwa kiwango hatari.

Kaunti hizo ni pamoja na Garissa, Mandera, Mombasa, Wajir na Makueni miongoni mwa zingine.

Mafuriko yanayoshuhudiwa nchini kufuatia mvua za El Nino yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 70 huku zaidi ya wengine 35,000 wakiachwa bila makazi.

Wengi wa waathiriwa hawana chakula wala bidhaa zingine za matumizi kama vile matumizi, hali ambayo imesababisha wafanyabiashara kuhodhi chakula.

Gavana wa kaunti ya Garissa Nathif Jama wafanyabiashara dhidi ya kuhodhi chakula akionya kuwa yeyote atakayepatikana atachukuliwa hatua kali.

 

 

 

 

 

 

Share This Article