Idadi ya watahiniwa waliopata Gredi ya C- kurudi chini iliongezeka katika mtihani wa kidato cha nne, KCSE wa mwaka 2024.
Kulingana na matokeo yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu Julius Ogamba leo Alhamisi, jumla ya watahiniwa waliopata Gredi ya C- kurudi chini ni 476,889.
Hii ni ikilinganishwa na watahiniwa 401,216.
Kulingana na matokeo hayo, watahiniwa 111,717 walipata Gredi ya C, C- (118,781), D+ (128,885), D (153,334), na D- (151,487).
Watahiniwa 48,333 waliambulia Gredi ya E.
Hiyo ina maana kuwa watahiniwa hao watalazimika kujiunga na vyuo na taasisi zingine za mafunzo ya kiufundi.
Hata hivyo, wana chaguo la kurudia tena kidato cha nne ili kuwinda matokeo bora.
Baraza la Kitaifa la Mitihani nchini, KNEC linasema mtihani wa mwisho wa KCSE utafanywa mwaka 2027.