Idadi ya waliofariki kwenye ajali ya Kakamega yafika 13

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 10 wafariki katika ajalai ya barabarani Kakamega.

Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya barabarani katika kituo cha kibiashara cha Iguhu, kaunti ya Kakamega yafika 13.

Gavana wa Kakamega Fernandez Barasa, alisema watu watatu zaidi walifariki wakipokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Kakamega.

Akizungumza alipowatembelea manusura wa ajali hiyo hospitalini, Gavana huyo alitoa wito kwa wanaotumia barabara kuwa makini zaidi

Watu 10 walifariki jana katika ajali hiyo ya barabarani iliyohusisha magari mawili ya abiria yaliyokuwa yakielekea Kisumu na lori la kubeba mafuta lililokuwa likielekea Kakamega.

Wakati huo huo, Jamaa na marafiki wa waathiriwa wa ajali hiyo,  leo Alhamisi walifika katika chumba cha maiti cha Kakamega kutambua miili ya wapendwa wao.

Wakiwa na huzuni kubwa, jamaa hao walielezea matukio ya mwisho wakiwa na wapendwa wao kabla ya ajali hiyo iliyotokea katika kituo cha kibiashara cha Iguhu.

Watu 20 waliojeruhiwa katika ajali hiyo wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kakamega, ile ya Iguhu na Mukumu.

TAGGED:
Share This Article