Huku taifa hili likishuhudia wimbi la mauaji dhidi ya wanawake, biwi la simanzi lilitanda leo katika kijiji cha Kasist kaunti ya Baringo, baada ya majirani kupata mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka 21,ukimwa umeoza.
Mwili huo ulipatikana katika chumba kinachodaiwa kuwa cha mumewe.
Wakazi hao waliwapasha polisi habari, ambao walifika na kuuchukua mwili huo.
Hata hivyo mumewe mwanamke huyo anyejulikana kama Kipsang’, alitiwa nguvuni, huku akitajwa mshukiwa mkuu katika mauaji hayo.
Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Baringo Kaskazini Mohamed Abdi alisema, “Tulipokea taarifa kwamba mwili wa mwanamke ulimefungiwa chumbani. Tulipofika, tulipata kuwa kuna uwezekano mwanamke huyo alifariki siku tatu zilizopita. Polisi waliuuchukua na kuupeleka kwenye chumba cha wafu naye mshukiwa anazuiliwa na polisi uchunguzi ukiendelea.”
Inadaiwa mauaji hayo yalitokana na tofauti za kimapenzi.