Idadi kubwa ya wanafunzi warejea shuleni Baringo

Dismas Otuke
1 Min Read

Idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na shule katika kaunti ya Baringo imerekodiwa kufuatia kuimarika kwa hali ya usalama eneo la North Rift.

Wanafunzi wengi waliokuwa wametoroka masomo kutokana na wizi wa mifugo uliozorotesha usalama wameonekana wakirejea kutokana na juhudi za wanajeshi wa Kenya.

Wanajeshi hao wameongoza ujenzi wa madarasa na kupambana na wezi wa mifugo katika opereshini ijulikanayo kama Operesheni Maliza Uhalifu (OMU).

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwa wanajeshi wa KDF, baadhi ya shule zilizonakili ongezeko la wanafunzi wanaorejea kwa masomo ni Arabal, Kapindasum, Mukutani, Chemoril na  Chesitet huku pia jamii za maeneo hayo zikirejelea maisha ya kawaida.

Kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Arabal Joel Kipkwony, wanafunzi katika kaunti za Baringo na Laikipia wameanza masomo vyema.

Akiwahutubia wanafunzi katika shule ya msingi ya  Chemoril, Brigedia S M Huria, ambaye ni Kamanda OMU amewahimiza walimu na wanafunzi  kuwa mabalozi wema wa amani.

Share This Article