Ibada ya wanafunzi waliofariki Hillside Endarasha Academy yafanyika Nyeri

Dismas Otuke
1 Min Read

Ibada kwa ajili ya wanafunzi 21 walioangamia kwenye mkasa wa moto shuleni Hillside Endarasha Academy katika kaunti ya Nyeri inafanyika hii leo Alhamisi katika uwanja wa Mweiga.

Naibu Rais Rigathi Gachagua na viongozi wa upinzani akiwemo Kalonzo Musyoka ambaye ni kinara wa chama cha Wiper ni miongoni mwa wanaohudhuria ibada hiyo.

Ibada hiyo, ambayo awali ilipangwa kufanyika juzi Jumatano, iliaihirishwa hadi leo na waandalizi wa hafla hiyo kutokana na kile walichokitaja kuwa sababu maalum.

Wanafunzi hao 21 walikuwa miongoni mwa wavulana wengine 150 waliokuwa wamelala kwenye bweni wakati moto ambao haujabainika chanzo chake ulipoteketeza bweni hilo.

Naibu Rais Rigathi Gachagua anatarajiwa kuongoza ibada hiyo ambayo pia itahudhuriwa na maafisa kutoka wizara ya Elimu, wazazi na jamaa na marafiki wa walioangamia.

Uchunguzi kuhusu mkasa huo wa moto ulioendeshwa na maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai, DCI bado haujafichua chanzo.

 

Share This Article