Ndege moja ya vikosi vya ulinzi hapa nchini KDF, imeanguka katika eneo la Sindar, kaunti ya Elgeiyo Marakwet.
Ajali hiyo ilitokea Alhamisi alasiri, muda mfupi baada ya helikopta hiyo kung’oa nanga katika uwanja wa shule ya upili ya wavulana ya Cheptulel.
Maafisa wa KDF walikuwa katika shule hiyo kukadiria hali ya usalama, pamoja na mikakati iliyowekwa ya ufunguzi wa shule katika mpaka wa Pokot Magharibi na Marakwet.
Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, ndege hiyo ilishika moto baada ya kuanguka.
Tutawaletea habari zaidi kuhusu ajali hiyo……