Msanii wa muziki nchini Tanzania Harmonize amesema kwamba upasuaji wa kuimarisha urembo ni jambo la kawaida.
Alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya wanahabari pembezoni mwa onyesho lake na Nandy katika eneo la burudani la 1245.
Mojawapo ya maswali aliyoulizwa ni kuhusu mrembo Malaika aliyepokea tuzo kwa niaba yake kwenye tuzo za TMA ambapo alisema kwamba ni mrembo na amebeba zigo apendavyo.
“Haijalishi kama umbo ni la upasuaji?” aliuliza mwanahabari mmoja ambapo Harmonize alijibu akisema ni jambo la kawaida na litakuwa kueleweka hivyo katika muda wa miaka michache ijayo.
Kuhusu mahusiano, Harmonize alisema kwamba yuko pweke kwa sasa, hata baada ya uvumi kuenea kwamba amerudiana na mpenzi wake wa awali, Kajala.
Alifichua pia kwamba yeye huwa haandiki nyimbo zake bali huwa anaimba tu na kurekodi matukio ya maisha yake.
“Nikiimba wimbo wa furaha jua nina furaha, ukinifurahisha nakuimba, ukiona naimba nyimbo nzuri za mapenzi jua kuna mtoto nampenda” alisema msanii huyo.
Harmonize anaamini kwamba atakuwa mmoja wa washindi wa tuzo za Grammy katika awamu ijayo, baada ya wimbo wake “Single Again” kukosa kuteuliwa kuwania tuzo hizo awamu hii.