Harambee Starlets yaimarisha mazoezi kwa mechi ya kufuzu kombe la Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya kwa wanawake ,Harambee Starlets,inaendeleza mazoezi ya kambi kujiandaa kwa mechi ya kufuzu kombe la Afrika dhidi ya Cameroon.

Kambi hiyo ya mazoezi itaingia siku ya tano Alhamisi huku wachezaji 23 wakitarajiwa kuendeleza mazoezi ilivyokuwa Jumatano.

Starlets waliishinda Police FC bao moja kwa nunge katika pambano la kujipiga msasa Jumatano jioni katika uwanja wa Kasarani.

Kenya chini ya ukufunzi wa kicha Beldine Odemba itaondoka nchini Septemba 19, kuelekea Doula Cameroon kwa mkondo wa kwa za raundi ya kwanza kufuzu kwa kombe la Afrika dhidi ya wenyeji Ijumaa ijayo.

Mchuano wa marudio utasakatwa Kenya tarehe 26,huku mshindi akifuzu kwa raundi ya pili atakapomenyana na aidha Gabon au Botswana.

Fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wanawake zitaandaliwa mwaka ujao nchini Morocco.

Share This Article