Timu ya taifa ya Kenya ya wanawake,Harambee Starlets imeweka hai matumaini ya kunyakua kombe la CECAFA, baada ya kuwalabua Sudan Kusini, mabao 4-0 katika mchuno uliopigwa katika uchanjaa wa Azam Complex ,jijini Dares Salaam,Tanzania.
Faith Mboya alifungua ukurasa wa magoli kwa Kenya kunako dakika ya 3, kabla ya Violet Wanyonyi,Martha Amunyolet na Elizabeth Ochaka, kuongeza bao moja kila mmoja katika dakika za 47,66 na 95 mtawalia.
Kenya wanaongoza kundi A kwa pointi 9 watashuka uwanjani Jumamosi dhidi wenyeji Twiga Stars, huku mshindi akitwaa kombe.