Timu ya taifa ya soka ya kina dada ya Kenya, Harambee Starlets imewasili mjini Gaborone, Botswana Jumapili jioni kwa marudio ya mechi ya kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao.
Mchuano huo utapigwa Jumanne jioni huku Kenya wakihitaji ushindi ili kufuzu kwa fainali za kombe la Afrika mwakani nchini Morocco.
Wenyeji wanawinda sare tasa ili kufuzu baada ya kwenda sare ya 1-1 katika mkumbo wa kwanza jijini Nairobi.