Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets itafungua kampeni ya kuwania kombe la CECAFA dhidi ya Burundi leo jioni katika uwnaja wa Azam Complex jijini Dares Salaam ,Tanzania.
Burundi watakuwa wakishiriki mchuano wa pili mashindanoni baada ya kuwalaza Uganda bao moja kwa bila katika mechi ya ufunguzi.
Katika pambano jingine la Jumapili, Uganda watakabiliana na Sudan Kusini.
Harambee Starlets watarejea uwanjani kwa mchuano wa pili Juni 17 dhidi ya Uganda na mechi ya tatu dhidi ya Sudan Kusini, kabla ya kufunga ratiba dhidi ya wenyeji Tanzania tarehe 21 mwezi huu.
Mashindano hayo yanashirikisha mataifa matano huku timu mbili bora zikikutana kwenye fainali.