Hamas yasema hakuna lililoafikiwa katika mazungumzo ya kusitisha vita Gaza

Marion Bosire
1 Min Read

Kundi la Hamas limesema kwamba hakuna lolote limeafikiwa katika mazungumzo na Israel ya kusitisha vita Gaza huku wananchi wengi wa Israel wakiandamana katika jiji la Tel Aviv wakitakaserikali iokoe mateka na kuafikia mkataba.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo kwa jina Osama Hamdan, anayeishi Lebanon, alisema kundi lake liko tayari kufanya mazungumzo kuhusu mapendekezo ya kusitisha mapigano ambayo yamedumu miezi 9.

Wapatanishi waarabu wanaoungwa mkono na Marekani wamekosa kuafikia ufanisi katika mazungumzo ya kusitisha vita huku pande mbili husika za vita hivyo zikinyosheana kidole cha lawama.

Hamas inasisitiza kwamba mkataba wowote utakaoafikiwa ni lazima umalize mapigano kabisa na kuhakikisha wanajeshi wa Israel wanaondoka Gaza kikamilifu.

Israel kwa upande wake inataka mkataba ambao utatoa fursa kwa kusitisha vita kwa muda kila mara hadi pale ambapo kundi la Hamas ambalo limetawala Gaza tangu mwaka 2007 litamalizwa kabisa.

Huku hayo yakijiri, mapigano yameendelea kati ya wanajeshi wa Israel na wapiganaji wa kipalestina katika eneo la Shujayea kati jiji la Gaza.

Shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia wakimbizi wa Palestina UNRWA limeonye kuhusu hali ambayo inazidi kudorora ya wakimbizi huku joto likiongezeka sawa na takataka na maji taka.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *