Hali imekuwa tete katika mji wa Kivu Kaskazini katika Jamhuri ya Kidemokrwasia ya Congo, DRC baada ya waasi wa M23 kutwaa miji miwili.
Mapigano makali yaliripotiwa Jumamosi iliyopita huku mamia wakitoroka makwao wakati waasi hao wa M23 walipotwaa miji ya Masisi na Lushebere mashariki mwa DRC.
Polisi nchini humo waliwazuaia waasi kuingia mjini Nyirangongo na kuelekea mjini Goma, ambapo yamkini walifanikiwa kuingia mjini Masisi.
Kwa mujibu wa msemaji wa serikali Patrick Muyaya, mapigano hayo mapya yamesababisha raia wengi kutoroka makwao.
Serikali ya DRC imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kushirikiana na kundi hilo la waasi wa M23.