Hali ingali tete nchini Haiti licha ya kubuniwa kwa serikali ya mpito

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali mpya ya mpito iliyobuniwa nchini Haiti chini ya wiki  moja iliyopita inakabiliwa na changamoto huku Waziri Mkuu mpya  Fritz Bélizaire, akionekana  kukataliwa na  wajumbe wengi wa jopokazi.

Uteuzi wa awali wa Michael Patrick kuwa Waziri Mkuu ulibatilishwa na wanachama wanne kati ya saba walio na uwezo wa kupiga kura kwenye baraza hilo la wajumbe tisa, huku wanachama wengine wakijitenga na Bélizaire wakidai kutomfahamu .

Hatua hiyo imezua tumbojoto na mgawanyiko kwenye baraza hilo ,huku wanachama wengine wanaopinga uteuzi wa Bélizaire aliyehudumu kama Waziri wa michezo  kati ya mwaka 2006 na 2022 wakitishia kujiuzulu.

Haiti imezama kwenye lindi la machafuko tangu Februari 29 huku magenge ya majangili yakiwauwa rai kiholela na kuachiliwa huru kwa wafungwa 4,000, kutoka magereza kadhaa ya jijini kuu la Port Au Prince.

TAGGED:
Share This Article