‘Hakuna mpango wa kuhamisha AFCON’,asema Motsepe

Fainali za AFCON zimeratibiwa kuandaliwa kati ya Juni 19 na Julai 17 mwaka ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe amesema hakuna mpango wa kuhamisha mashindano ya kombe la mataifa mwakani (AFCON) kutoka kwa mataifa ya Kenya,Uganda na Tanzania.

Motsepe amesema hayo Alhamisi alipowasili Dar es Salaam na kukagua ukarabati wa uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkappa .

Baadaye kinara huyo atazuru Nairobi kukagua viwanja vya Kasarani na Talanta, kabla ya kuhitimishia ziara Kampala ,Uganda.

Akizungumza na Wanahabari huko Dar,Motsepe amekiri kuwa ingawa matayarisho yako nyuma kwa Kenya,Tanzania na Uganda, huku ikisalia meizi mitatu kabla ya kuanza kwa kipute hicho,hakuna mwandalizi mbadala na mashindano hayo yatafanya ilivyoratibiwa.

Aidha,kinara huyo alikiri kuona mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu matayarisho ya Tanzania,akielezea imani ya kila kitu kuwa tayari kwa wakati ufaao.

Fainali za AFCON zimeratibiwa kuandaliwa kati ya Juni 19 na Julai 17 mwaka ujao.

Share This Article