George Kamal aondoka KQ baada ya kukamilika kwa muhula wake

Shirika la KQ lilimtakia mema anapofungua ukurasa mpya maishani, likitarajia kuwa uongozi wake na mchango wake utaendelea kuwa wenye manufaa katika sekta ya safari za ndege.

Tom Mathinji
1 Min Read
Dr. George Kamal, aondoka Kenya Airways baada ya kukamilika kwa muhula wake.

Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ), limemuaga kaimu Mkurugenzi Mkuu, aliyepia Afisa Mkuu Mtendaji anayeondoka Dr. George Kamal, baada ya muhula wake wa kuhudumu kukamilika.

Chini ya uongozi wa Dkt. Kamala, KQ imesema ushirikiano wake na operesheni zake ziliimarika pakubwa na kutimiza lengo lake la kuunganisha bara Afrika na sehemu zingine za dunia.

“Tunamshukuru Dkt. George Kamal kwa uongozi wake, utoaji huduma na kujitolea kwake kwa Kenya Airways, pamoja na kuwahudumia wateja wetu na sekta nzima ya safari za ndege,” ilisema taarifa ya Kenya Airways kupitia ukurasa wa X.

Shirika la KQ lilimtakia mema anapofungua ukurasa mpya maishani, likitarajia kuwa uongozi wake na mchango wake utaendelea kuwa wenye manufaa katika sekta ya safari za ndege.

“Shukran sana Dkt. George Kamal, kwa huduma zako na kujitolea kwa shirika la Kenya Airways. Tunakutakia kila la heri katika safari yako inayofuata,” iliongeza taarifa hiyo.

Share This Article