Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula, amesema hali ya amani miongoni mwa jamii za wafugaji, imefanikisha eneo la kaskazini mwa nchi kupiga hatua katika elimu, biashara na uwekezaji.
Wetang’ula, alisema ushirikiano kati ya serikali, kanisa Katoliki, wazee na jamii za eneo hilo, umepunguza mizozo kati ya Pokot ,Turkana na jamii jirani.
“Amani ni msingi wa maendeleo. Wakati jamii zinaishi pamoja kwa amani, zinapata fursa ya kufanya biashara, watoto wao wanapata elimu, wanawekeza na kushiriki kikamilifu kwa maendeleo ya eneo hilo,” alisema Mudavadi.
Aliyasema hayo katika kanisa katoliki la St Anthony, eneo bunge la Sigor, kaunti ya Pokot Maghaibi, ambako alipongeza kanisa katoliki kwa jukumu lake la kuleta amani na upatanishi katika jamii.
Alitoa wito wa juhudi hizo za kuleta amani zitapuniliwe hadi katika kaunti zingine zilizo na wafugaji wa kuhamahama, ikijumuisha kaunti za Pokot Magharibi, Samburu, Baringo na Turkana.