Rais William Ruto amesema bara la Afrika linaendelea kushirikiana kwa karibu na Kamandi Kuu ya Marekani Afrika, ili kukabiliana na hatari za kimataifa.
Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi, kiongozi wa taifa alisema ushirikiano huo utafanikisha pakubwa kusambaratisha makundi ya itikadi kali, utashughulikia dharura na kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu.

“Ushirikiano huu ni muhimu sana kwa bara hili kwa sababu amani, udhabiti na usalama ni vigezo muhmu kwa maendeleo, utangamano, biashara na ufanisi,” alisema Rais Ruto.
Aliyasema hayo aliposhiriki mazungumzo na Kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani barani Afrika (AFRICOM) Jenerali Dagvin Anderson, aliyeandamana na balozi wa Marekani hapa nchini Susan Burns.