Idadi ya waliofariki kwenye tetemeko la ardhi Japani yafika 13

Waziri Mkuu wa Japan, Sanae Takaichi, amesema watu kadhaa hawajulikani walipo na huenda wamekwama kwenye vifusi wakisubiri kuokolewa.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 13 wafariki kwenye tetemeko la ardhi Japan.

Idadi ya waliofariki kwenye tetemeko la ardhi nchini Japan imefika 13, huku wanajeshi na maafisa wa  kushughulikia dharura wakiendelea kuwatafuta manusura kwenye vifusi vya majengo.

Huduma za treni na huduma kwenye baadhi ya viwanja vya ndege zimesitishwa, serikali ikiendelea kukadiria uharibifu uliosababishwa na tetemeko hilo la kipimo cha 7.1 kilichokumba eneo la Kumamoto, kusini mwa Japani.

Waziri Mkuu wa Japan, Sanae Takaichi, amesema watu kadhaa hawajulikani walipo na huenda wamekwama kwenye vifusi wakisubiri kuokolewa.

“Kuna watu ambao wanasubiri kuokolewa na muda unazidi kuyoyoma….tutaenda sote kuwatafuta na kuwaokoa watu wengi iwezekanavyo,” alisema Takaichi.

Takriban nyumba  36,900 hazina umeme, nyumba 9,500 zikikosa umeme, huku mitanao ya mawasiliano ikikatika katika baadh ya sehemu, hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa serikali Minoru Kihara.

Share This Article