CNN, MS NOW na Politico vyapigwa marufuku White House

Trump alisema marufuku dhidi ya vituo hivyo, imesababishwa na taarifa kadhaa katika muda wa miaka miwili iliyopita.

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Marekani Donald trump kwenye mkutano wa awali na wanahabari.

Rais wa Marekani Donald Trump amepiga marufuku mashirika ya habari ya CNN, MS NOW na Politico katika Ikulu ya White House, akiyashtumu kwa kueneza habari potovu kuhusu utawala wake.

“Ninafuraha kutangaza kuwa napiga marufuku mara moja CNN, MSNOW na Politico katika White House, kutokana na kuendelea kwao kuripoti habari za uwongo,’ alisema Rais Trump kupitia ukurasa wake wa Truth.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 80 na ambaye hajakuwa na uhusiano mzuri na baadhi ya vyombo vya habari, alionya kuwa mashirika mengine ya habari yatachukuliwa hatua sawia na hiyo, lakini hakuyataja.

Alipoulizwa ikiwa kuna taarifa ambayo ilisababisha kuchukuliwa kwa hatua hiyo, Trump alisema marufuku dhidi ya vituo hivyo, imesababishwa na taarifa kadhaa katika muda wa miaka miwili iliyopita.

Muda mfupi baada ya marufuku hiyo, Shirika la CNN lililaani hatua hiyo likiitaja kuwa kinyume cha sheria na ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari nchini Marekani.

Share This Article