Kagwe ahimiza kuchungwa upya kwa kodi zinatozotwa kilimo cha maua

Kagwe alisema kilimo cha maua ni mojawapo ya nguzo kuu za nchi hii katika kuleta pato la kigeni.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mutahi Kagwe - Waziri wa kilimo na Ustawi wa Mifugo.

Waziri wa Kilimo na Ustawi wa Mifugo Mutahi Kagwe, ametoa wito wa kuchunguzwa upya kwa baadhi ya kodi zinazotozwa mazao ya kilimo cha maua.

Kagwe alidokeza kuwa gharama za juu za uzalishaji maua, zinahujumu imani ya wawekezaji katika sekta hiyo.

Akizungumza katika maonyesho ya kilimo cha maua yanayoendelea mjini Naivasha, waziri huyo alisema kilimo cha maua ni mojawapo ya nguzo kuu za nchi hii katika kuleta pato la kigeni.

Kulingana na waziri huyo, baadhi ya ushuru kutoka kwa serikali ya taifa na zile za kaunti, zinaweza ondolewa ili wakulima wapate faida zaidi kutokana na kilimo hicho.

“Nitajadiliana na Mawaziri wenzangu wa Hazina Kuu na wa Biashara kuhusu haja ya kuchunguza upya baadhi ya ushuru kwenye sekta ya maua, ambazo zinahujumu ukuaji wa sekta hiyo muhimu.

Kagwe alisema serikali inashirikiana kwa karibu na Muungano wa Ulaya kuhusu masharti ya usafi na afya ya mimea pamoja na viwango vingine vya usalama vinavyoathiri bidhaa zinazouzwa nje ya nchi.

TAGGED:
Share This Article