Gavana Ntutu azindua pikipiki 34 na magari 2 kuboresha utoaji huduma

Martin Mwanje
1 Min Read

Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ole Ntutu amezindua pikipiki 34 na magari 2 kwa lengo la kuimarisha utoaji huduma kwa raia katika kaunti hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyia katika makao makuu ya kaunti, Ole Ntutu alisisitiza wajibu muhimu unaotekelezwa na maafisa wa utawala wa wadi katika utawala wake.

Amewataja maafisa hao kuwa muhimu katika kuratibu sera na miradi ya kaunti katika ngazi ya wadi, na hivyo kuwa daraja muhimu linalounganisha jamii na serikali ya kaunti.

“Maafisa hawa wa utawala ndilo daraja kati ya serikali ya kaunti na jamii, wakiwahudumia watu kila siku,” alisisitiza Gavana Ole Ntutu.

Serikali ya kaunti ya Narok imewekeza shilingi milioni 14 katika ununuzi wa pikipiki na magari hayo yatakayohakikisha maafisa hao wanafika kila pembe ya kaunti hiyo kuwahudumia raia.

Share This Article