Gavana wa kaunti ya Narok Patrick Ole Ntutu amempongeza Rais William Ruto kwa kuteua mawaziri wapya kutoka upinzani serikalini.
Hasa, ameelezea kufurahia kwake kutokana na kujumuishwa kwa kwa jamii ya Wamaasai serikalini kutokana na kuteuliwa kwa Soipan Tuya kuwa Waziri wa Ulinzi.
Akizungumza katika kijiji cha Oletukat, Gavana Ntutu alitumia fursa hiyo kusifia baraza hilo alilolitaja kuwa jumuishi kwa kuwaleta Wakenya wote pamoja.
Ntutu pia alisisitiza haja kwa wazazi kuzungumza na watoto wao wakati huu wa likizo ili kuepukana na mimba za mapema.
Semi zake ziliungwa mkono na mwakilishi wa wanawake katika kaunti hiyo Rebecca Tonkei aliyetambua pia juhudi za serikali ya kaunti hiyo kuimarisha bei ya maziwa.