Maafisa wa Huduma ya Taifa ya Polisi, wamemkamata mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarati katika kaunti ya Vihiga.
Mshukiwa huyo alikamatwa akiwa na kilo tatu za bangi kilo moja ya tumbaku na karatasi za plastiki, baada ya maafisa wa polisi kutekeleza operesheni kali katika kituo cha kibiashara cha Majengo.
Kupitia ukurasa wa X, Huduma ya Taifa ya Polisi, ilisema kwa sasa mshukiwa huyo anazuiliwa katika korokoro za polisi akisubiri kufikishwa mahakamani.
“Huduma ya Taifa ya Polisi haitalegeza kamba katika vita dhidi ya mihadarati. Tunazidi kushirikiana na jamii na wadau wengine kulinda maslahi ya umma,” ilisema NPS kwenye mtandao wa X.