Gavana Barasa ataka uwanja wa ndege wa Kakamega ufanyiwe ukarabati

Tom Mathinji
1 Min Read
Uwanja wa ndege wa Kakamega.

Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa,  ametoa wito kwa wizara ya uchukuzi na miundomsingi kushughulikia haraka changamoto za miundomsingi zinazokumba uwanja mdogo wa ndege wa Kakamega.

Wito wa Gavana huyo unajiri baada ya kampuni ya uchukuzi wa ndege ya Skyward Express, kusema itasimamisha safari zake kwenye uwanja huo kuanzia Septemba 30,2024, kutokana na hali duni ya eneo la kutua ndege la uwanja huo.

Kampuni  ya Fly Skyward express kupitia arifa kwa umma, ilitangaza kusitishwa kwa safari zake za Kakamega kutokana na hali duni ya uwanja huo wa ndege.

“Tunasikitika kutanga kuwa kuanzia Septemba 30, 2024, tunasitisha kwa muda safari zetu za ndege kutoka na kuingia Kakamega, kutokana na hali duni ya uwanja huo wa ndege, ambao hautimizi viwango vyetu vya ubora,” ilisema kampuni ya Fly Skyworld kupitia mtandao wa X siku ya Jumamosi.

Kulingana na Gavana huyo aliyezungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la PAG Sichirayi eneo la Lurambi, alisema kusitishwa kwa safari hizo za ndege kutaathiri pakubwa  uchumi wa kaunti hiyo.

Share This Article