Gavana Achani azindua miradi ya ukarabati wa barabara

Tom Mathinji
1 Min Read
Gavana wa Kwale Fatuma Achani azindua miradi ya ukarabati wa barabara.

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani, amezindua miradi ya ukarabati wa barabara katika kaunti hiyo, kwa lengo la kuimarisha na kufanikisha shughuli za uchukuzi.

Kulingana na Achani, barabara zilizolengwa ni  pamoja na ile ya Kona ya polisi hadi hospitali ya rufaa ya Msambweni pamoja na barabara ya Mwangwei hadi Majoreni, katika eneo bunge la Lungalunga ambazo zitawekwa lami.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Achani alisema miradi hiyo itatekelezwa kwa awamu ambapo katika awamu ya kwanza barabara ya Mwangwei hadi Majoreni imetengewa shilingi milioni 97, na ile ya Kona polisi hadi hospitali ya rufaa ya Msambweni ikitengewa shilingi milioni 74.

Kiongozi huyo amewataka wakandarasi wa miradi hiyo kuhakikisha wanatekeleza ujenzi huo kulingana na maelezo ya mkataba huku akiwataka kuwapa kipaumbele vijana wa maeneo husika katika nafasi za ajira.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *