Gathimba atwaa ubingwa katika mkondo wa nne wa Afraha,Nakuru

Jumla ya wanariadha 256 walishiriki fainali hiyo ya mita 5,000.

Dismas Otuke
2 Min Read

Bingwa wa zamani wa Afrika Samuel Gathimba wa Magereza alishinda mbio za kilomita 15 matembezi  kwa saa moja, dakika 3 na sekunde 12, katika siku ya  mwisho ya  mkondo wa nne wa mashindano ya chama cha Riadha Kenya, uwanjani Afraha, Nakuru.

Wilberforce Kones wa Polisi alishinda mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwa wanaume kwa  muda wa dakika 8 na sekunde 45,  akifuatwa na Peter Langat na Wesley Rono, wote kutoka North Rift, katika nafasi za pili na tatu kwa dakika 8 sekunde 46.6 na dakika 8 sekunde 54.1 mtawalia.

Simon Mungai wa Central ameshinda mbio za mita 5,000, baada ya kuzitimka kwa dakika 13 sekunde 30.9, akifuatwa na Dennis Kemboi, kutoka kilabu cha Konoin kwa dakika 13 sekunde 36.2, huku Festus Kaptum wa kambi ya Sinonin akiridhia nafasi ya tatu kwa dakika 13 sekunde 43.8.

Jumla ya wanariadha 256 walishiriki fainali hiyo ya mita 5,000.

Aron Chemingwa ameibuka bingwa wa mita 800 akitumia dakika 1 sekunde 45.1, akifuatwa na Shadrack Kimtai na Dominic Kiptoo, katika nafasi za pili na tatu kwa dakika 1 sekunde 45.6 na dakika 1 sekunde 46.5.

Caren Chepchirchir kutoka kilabu ya Nala alishinda mita 1,500 akitumia dakika 4 sekunde 15.9, akifuatwa na Rebecca Mwangi wa Central kwa dakika 4 sekunde 16.7 huku Naomi Korir wa Central Rift akiambulia nafasi ya tatu.

Sheila Chepkosgei wa Nairobi ndiye mshindi wa mita 800, akiziparakasa kwa dakika 2 sekunde 1.1, mbele ya Purity Chepkurui na Naumglorious Chepchumba, waliochukua nafasi za pili na tatu kwa dakika 2 sekunde 1.5 na dakika 2 sekunde 1.9 katika usanjari huo.

Zaidi ya wanariadha 2,000 walishiriki mkondo huo wa nne.

 

Website |  + posts
Share This Article