Gachagua: Nimefanikiwa kuunganisha Mlima Kenya

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Rigathi Gachagua.

Naibu Rais Rigathi Gachagua, amesema juhudi zake za kuunganisha eneo la Mlima Kenya zimezaa matunda.

Huku akiwashutumu wale wanaopinga juhudi zake, Gachagua  alisema hatachoka kuwafikia viongozi wote kwa ajili ya umoja wa kitaifa.

“Umoja wa eneo la Mlima hauyumbishwa na umekamilika. Ni asilimia moja tu ya viongozi iliyosalia na watajiunga nasi,” alisema Gachagua.

Akizungumza leo Ijumaa wakati wa kutawazwa kwa kasisi Benson Gathungu almaarufu Kiengei wa kanisa la JCM katika kaunti ya Kiambu, Gachagua alisema anashirikiana na wazee kuwatafuta marafiki wapya.

“Hatuungani dhidi ya yeyote au eneo lolote. Ni kwa maslahi yetu ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. Mtu yeyote hapaswi kuwa na hofu,” alidokeza naibu huyo wa Rais.

Gachagua alihusisha ufanisi katika kuunganisha eneo la Mlima Kenya na hatua yake ya kuwakumbatia viongozi wote bila kujali miegemeo yao ya kisiasa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

“Hatupigani na yeyote, tunatafuta urafiki kutoka kila sehemu. Tunawahimiza viongozi wasiwashambulie wengine ila wafanyekazi pamoja,” alisema Gachagua.

Aidha alitoa wito kwa viongozi waliochaguliwa  kuwaheshimu wakenya, na kuangazia kuwahudumia na kuimarisha maisha yao.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *