Naibu Rais Rigathi Gachagua leoAlhamisi alifungua mkutano wa wabunge kuhusu utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi jijini Nairobi.
Gachagua alisema kwamba mabadiliko ya tabia nchi ni tishio kubwa kwa uwepo wa binadamu na hivyo kila juhudi zinazolenga kupiga jeki mipango ya kupambana na hali hiyo itafadhiliwa na serikali.
Alifurahia kwamba wabunge wamechukua hatua ya kuongoza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Mkutano wa leo ni wa kuzindua mpango makhsusi wa kundi la wabunge kuhusu mazingira na mabadiliko ya tabia nchi. Mpango huo ni wa jinsi wataangazia utunzi wa mazingira, kulinda maliasili na kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Naibu Rais alilakiwa katika hoteli ya Sarova na waziri wa mazingira Soipan Tuya na naibu spika wa bunge la seneti Kathuri Murungi kati ya viongozi wengine.