Watu wapatao 3,500 kutoka kaunti za Makueni na Nairobi watanufaika kwa huduma za matibabu ya meno bila malipo kwa siku nne zijazo.
Huduma hiyo ambayo imeandaliwa na na shirika la Mars Wrigley na chama cha Madaktari wa meno (KDA), katika maadhimisho ya siku ya kitaifa ya usafi wa mdomo iliyofanyika
Jana.
Shughuli hiyo ilianza Jumatatu katika kaunti ya Makueni eneo la Mbooni, ikiwashirikisha madaktari wa meno 700, kabla ya kukamilika jana katika mitaa ya Maringo na eneo bunge la Embakasi kusini.