Msanii wa Uganda Fille Mutoni alilazimika kufichua hali yake ya kiafya, kufuatia uvumi wa muda mrefu kumhusu.
Binti huyo anasema hana virusi vya ukimwi inavyodhaniwa ila mpenzi anavyo.
Fille alifichua wakati wa mwito kanisani nchini Rwanda siku chache zilizopita, akiongeza kwamba binti yao pia yuko salama.
“Nilipata mtoto na mwanamume aliyekuwa na wanawake watano na mimi nilikuwa wa sita. Kwa bahati mbaya, ameambukizwa na wanawake wengine lakini ninashukuru Mungu kwamba mimi na mtoto wangu tuko salama.” Alisema Fille katika ushuhuda wake.
Msanii huyo alifichua pia kuwa amekuwa huru kutokana na dawa za kulevya kwa miezi saba.
Alielezea kwamba alitumia dawa za kulevya kama kokeini, heroini na bhangi kwa miaka sita.
Ufichuzi huu hata hivyo haujamfurahisha Kats baba ya mtoto wa Fille anayesema kwamba Fille anatafuta tu kuhurumiwa na umma.
Kats ambaye ni mtangazaji wa runinga ametoa onyo kwa Fille asiwahi kuzungumzia familia yake.
“Watu wanapenda kucheza michezo ya huruma tu coz (soma kwa sababu) Nilinyamaza lakini nauliza jinsi ya kukabiliana na Miaka 7 ya uraibu wa dawa za kulevya na nini kinakuja nayo,” alisema kwenye mtandao wa X.
“Usiwahusishe watoto wangu wala mama zao jamaa hujawaona popote pale unapowahi kuzungumza na wanataka kuiweka hivyo. Clout akimfukuza ain’t good,” Kats aliongeza.