Mshindi wa nishani ya shaba ya dunia katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji Faith Cherotich, ameteuliwa kuwania tuzo ya mwanariadha chipukizi bora wa mwaka wa shirikisho la Riadha Duniani.
Cherotich pia ni mwanariadha mwenye kasi ya pili katika mbio hizo kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20, kwa muda wa dakika 8 sekunde 59 nukta 65.
Chipukizi huyo pia alimaliza wa nne katika mbio za nyika duniani kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20.
Cherotich atawania tuzo hiyo pamoja na
Medina Eisa wa Ethiopia na Angelina Topic, wa Serbia.