EACC yashinikiza uthibitishaji mkali wa vyeti ya masomo

Martin Mwanje
1 Min Read
Meneja wa EACC wa Kanda ya Magharibi, Eric Ngumbi

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imetoa wito kwa vyuo vikuu, vyuo, taasisi za kusimamia mitihani na asasi zingine za udhibiti wa sekta ya elimu kuimarisha mifumo ya uthibitishaji wa mifumo ya mitihani na ustahilifu. 

Lengo ni kudhibiti kughushi kwa vyeti kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Wito huo umetolewa na Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC Abdi Mohamud kupitia kwa Meneja wa Kanda ya Magharibi Eric Ngumbi wakati wa warsha ya Bunge la Bungoma iliyofanyika jijini Kisumu.

Mohamud amesisitiza umuhimu wa uthibitishaji mkali kufanywa kuhakikisha ni wanaofuzu kwa uwazi pekee ndio wanahudumu katika ofisi za umma.

Tume hiyo imeapa kukabiliana vikali na zimwi la kughushi vyeti vya masomo, ikiwa ni pamoja na kuwataka walioghushi vyeti kurejesha fedha na mafao mengine waliopata kupitia vitendo vyao ghushi.

Share This Article