Mafwele matatani kwa ‘kuwatesa’ wanaharakati wa haki za binadamu

Martin Mwanje
1 Min Read
Faustine Jackson Mafwele ambaye ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi nchini Tanzania

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi nchini Tanzania Faustine Jackson Mafwele hawezi kukanyaga guu nchini Marekani kwa sasa. 

Hii ni baada ya kuwekewa vikwazo na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Kwenye taarifa, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Marco Rubio amesema kwa kuzingatia taarifa za kuaminika, Mafwele alihusika katika ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

“Mwaka jana, jeshi la polisi liliwakamata, kuwatesa na kuwafanyia ukatili wa kingono raia wa Uganda Agather Atuhaire na raia wa Kenya Boniface Mwangi, waliokuwa jijini Dar es Salaam kufuatilia kesi mahakamani dhidi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu,” Rubio anaelezea kwenye taarifa hiyo.

Wanaharakati Agather Atuhaire wa Uganda na Boniface Mwangi wa Kenya / Picha kwa hisani ya Reuters

Serikali ya Tanzania haijazungumzia taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Share This Article