Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imerejesha kipande cha ardhi cha thamani ya shilingi 12, kilichokuwa kikimilikiwa na Kituo cha Polisi cha Karatina.
Kipande hicho kilikuwa kimetengewa ujenzi wa nyumba za maafisa wa polisi wa kituo cha Karatina, kaunti ya Nyeri.
Ardhi hiyo ya ukubwa wa ekari 0.074, yenye nambari ya usajili II/383, imekabidhiwa serikali baada ya kesi iliyodumu miaka 13 kortini.
EACC ilikuwa imewasilisha kesi kortini mwaka 2013 dhidi ya wastawishaji wa kibinafsi Joseph Mithamo Wachira, Peter Thinwa Ngari, John Muriuki Ruthuthi na Wilson Gacanja.
EACC imewataka wote wanaomiliki ardhi ya umma kuisalimisha la sivyo wahisi makali ya wembe sawia.
Tume hiyo katika siku za hivi karibuni imefanikiwa kurejesha ardhi kadhaa za umma zilizokuwa zimenyakuliwa na watu binafsi.