EACC yapongeza UNODC kwa kuunga mkono vita dhidi ya ufisadi nchini

Tom Mathinji
1 Min Read
EACC yapongeza Umoja wa Mataifa kwa kupiga jeki vita dhidi ya mihadarati hapa nchini.

Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi hapa nchini EACC, imelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mihadarati na Uhalifu UNODC, kwa kupiga jeki vita dhidi ya ufisadi hapa nchini na kanda nzima kwa jumla.

Akizungumza Jumatatu katika Makao Makuu ya EACC Jijini Nairobi, Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC Abdi Mohamud, alitambua msaada wa kisheria unaotolewa kwa tume hiyo kupitia ufadhili wa Muungano wa Ulaya, ambao alisema umeimarisha uwezo wa EACC kukabiliana na ufisadi.

Mohamud, pia alishukuru hatua ya UNODC ya kufungua kitovu cha kukabiliana na ufisadi barani Afrika hapa nchini Kenya, akidokeza kuwa hatua hiyo itatoa fursa nyingi kwa taifa hili na kanda hii kwa jumla.

Kwa upande wake, kiongozi wa ujumbe kutoka UNODC Ashita Mittal, alirejelea kujitolea kwa shirika lake kuendelea kuunga mkono juhudi za EACC za kuzuia na kukabiliana na ufisadi.

Alieleza haja ya kushirikiana kwa pamoja na vijana ili kukuza maadili kupitia kubuni vikundi vya maadili.

Aidha viongozi hao wawili walijadili utekelezwaji wa ushirikiano kati ya EACC na UNODC, pamoja na kubuni mikakati ya kuimarisha ushirikiano uliopo kwa sasa.

Website |  + posts
Share This Article