EACC yamwondolea lawama Ezra Chiloba

Tom Mathinji
1 Min Read
Ezra Chiloba.

Tume ya maadili na kukabiliana na ufisadi, EACC imemwondolea lawama aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya amwasiliano Ezra Chiloba kuhusiana na madai kasoro katika halmashauri hiyo.

Kulingana na tume hiyo uchunguzi ulibaini kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha wa kuthibitisha madai hayo dhidi ya Chiloba na maafisa wengine wa halmashauri hiyo.

Mnamo tarehe 26 mwezi Septemba mwaka 2023, tume hiyo ilipokea madai ya kasoro katika usimamizi wa mpango wa utoaji mikopo ya umiliki wa nyumba katika halmashauri ya mawasiliano nchini.

Ripoti kuhusu uchunguzi wa ukaguzi wa mpango huo uliotekelezwa kufuatia agizo la bodi tarehe 3 mwezi Mei mwaka 2023 ilipendekeza uchunguzi kuhusu Chiloba ili kujibu madai hayo.

Halmashauri hiyo ilimsimamisha kazi Chiloba katika wadhifa wa mkurugenzi mkuu na kumteua Christopher Wambua kwa kaimu mkurugenzi mkuu.

Kamati hiyo pia iliwasimamisha kazi maafisa wengine wane kwa madai ya usimamizi duni wa mpango huo ambapo serikali ilipoteza mamilioni ya pesa.

Chiloba ameteuliwa kuwa mkuu wa ubalozi mdogo wa Kenya huko Los Angeles nchini marekani.

TAGGED:
Share This Article