Duale: Hakuna mianya ya wizi wa mitihani

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri Aden Duale katika shule ya msingi ya Kahawa Garisson, Jijini Nairobi.

Waziri wa ulinzi Aden Duale, amesema maadili ya mitihani ya kitaifa ya mwaka huu  lazima ilindwe, huku mitihani ya shule za msingi iking’oa nanga kote nchini.

Alisema asasi zote za serikali zimeweka tahadhari ya hali ya juu kukabiliana na watakaojihusisha na wizi wa mitihani, aliosema watakabiliwa vilivyo.

Duale alizungumza katika shule ya msingi ya Kahawa Garrison, Jijini Nairobi baada ya kuongoza ufunguzi wa karatasi za mitihani za darasa la nane KCPE na tathmini ya gredi ya sita ya KPSEA.

Wanafunzi 165 katika shule hiyo wanafanya mtihani wa KCPE huku wanafunzi 172, wakifanya tathmini ya KPSEA

Waziri huyo alisema maadili na usalama wa mitihani ni muhimu kwa taifa hili, wani huwafanya wanafunzi kuwa wenye ushindani, sio tu hapa nchini mbali pia katika ngazi za Kimataifa.

“Mitihani ya kitaifa ni muhimu sana katika safari ya elimu ya wanafunzi wengi. Katika kipindi hiki muhimu zaidi, wanafunzi pamoja na wasimamizi wanahitaji usaidizi wetu,”alidokeza Duale.

Duale aliongeza kuwa,”Mitihani inapaswa kupewa maadili ya hali ya juu, na ndio maana tuko hapa kuhakikisha karatasi za mitihani hazijafunguliwa,”.

Mtihani wa mwaka huu wa KCPE unakamilisha miaka 38 ya mtaala wa elimu wa 8-4-4.

Share This Article