Waziri wa afya Aden Duale, ameteua kamati ya kutathmini madeni ya huduma za matibabu yanayodaiwa bima ya zamani ya afya NHIF .
Hatua hiyo inalenga kumaliza mrundiko wa madeni ya matibabu yanayodaiwa bima ya NHIF, iliyovunjiliwa mbali.
Kamati hiyo inajukumiwa na kukagua madeni yote ya hospitalini kati ya Julai 1 mwaka 2022 na Septemba 30 mwaka uliopita.
James Masiro ataongoza kamati hiyo akisaidiwa na Anne Wamae.
Wanachama wa kamati hiyo ni pamoja na Edward Kiplimo Bitok, Meshack Matengo, Meboh Atieno Awour, Tom Nyakaba, Catherine Karori Bosire, Paul Wafula, Catherine Mungania, James Oundo, Jackline Mukami Njiru, Judith Awinja na David Dawe.