Duale aitaka UNHCR kusitisha matumizi ya kuni katika kambi za wakimbizi

Rhobi Wenani
1 Min Read

Waziri wa mazingira Aden Duale ametoa changamoto kwa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi, UNHCR kusitisha ukataji wa miti ili kutumika kama kuni kwenye kambi za wakimbizi nchini Kenya.

Badala yake, Duale ameitaka UNHCR kutoa njia mbdala ya kawi kwenye kambi za wakimbizi zilizoko kaunti za Garissa,Turkana na Wajir badala ya ukataji miti.

Duale ameongeza amesisitiza umuhimu wa matumizi ya kawi safi  kulingana na sheria za Mamlaka ya mazingira nchini NEMA.

Alitaka kuhakikishwa kwamba kuwepo kwa mifumo dhabiti ya kuhakikisha utupaji taka kwa njia bora.

Duale ameongeza kuwa taklribani watu 20,000 wanashirikshwa katika mpango wa usafi na utunzaji mazingira

Aidha, waziri huyo pia inataja kwamba ili kuhakikisha utekelezaji wa kanuni hizi, kila kiwanda lazima kionyeshe thibitisho la utekelezaji wa amri ya mamlaka ya kudhibiti bidhaa za petroli (EPR), akionya kwamba iwapo kampuni itashindwa kufuata kanuni zilizowekwa, bidhaa zake zitapigwa marufuku na NEMA.

Rhobi Wenani
+ posts
Share This Article