Diamond azungumzia video zinazosambaa

Mwanamuziki huyo anahisi kwamba Rita aliamua kuvujisha video zao kama njia ya kumsaliti.

Marion Bosire
2 Min Read

Diamond Platnumz amepaaza sauti kuhusu video zinazosambaa mitandaoni zinazomwonyesha akiwa na binti kwa jina Rita Norbeth.

Video hizo zilichapishwa kwanza na Mange Kimambi na zinaonyesha Diamond na Rita wakiwa kwenye nyumba fulani huku wakipigana pambaja na mabusu.

Mwanamuziki huyo anasikika pia akimmiminia sifa Rita kwa urembo wake na umbo lake la kipekee.

Sasa Diamond kupitia Insta Stories anasema video hizo ni za mwaka 2023 na kwamba aliachana na Rita ambaye hamtaji kwa jina kwenye ujumbe huo.

“Nimeona Kuna clip zinasambazwa mtandaoni zinazonihusu…Clip hizo ni za zamani, mwaka 2023, na zina zaidi ya miaka miwili nyuma…Na Mwanamke huyo pia niliachana nae takriban miaka miwili sasa..” aliandika Platnumz.

Aliendelea kusema kwamba alimfahamisha mpenzi wake wa sasa ambaye anaaminika kuwa Zuchu kuhusu uhusiano huo na akamsamehe na wakaanza maisha mapya.

Mwanamuziki huyo anahisi kwamba Rita ndiye ameamua kusambaza video hizo akiziambatanisha na jumbe za uongo kama njia ya kumsaliti.

“Jambo hili lishafikishwa katika mamlaka husika na taratibu za Kisheria zinafuatwa. Shukran” alimalizia Diamond.

Mange Kimambi amechapisha jumbe za Whatsapp kati ya Rita na Diamond na tarehe inayoonekana humo ni 6 Mei, 2024 ambapo Rita anamwambia kwamba mapacha wao wanazidi kukua huku akiambatanisha ujumbe huo na picha za ujauzito.

Mwijaku mtangazaji na ambaye pia ni maarufu mitandaoni nchini Tanzania, anamshauri Diamond amshtaki Rita mahakamani akisema yeye pia aliwahi kufikwa na balaa kama hiyo na ikamalizikia mahakamani.

Wadadisi wengine wanahisi kwamba ni mgogoro gushi ambao wameanzisha kwa nia ya kuwafanya wengi wasiangazie ndoa ya Hamisa Mobeto aliyewahi kuwa mpenzi wa Diamond.

Hafla ya mwisho ya ndoa ya Hamisa na Aziz Ki inafanyika leo Februari 19, 2025.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *