Da Rest asajili kampuni yake ya kurekodi muziki na kusimamia wasanii

radiotaifa
1 Min Read

Mwanamuziki wa Rwanda Prince Ishimwe maarufu kama Da Rest, amesajili kampuni yake ya kurekodi muziki na kusimamia wanamuziki kwa jina ‘Eeey D Entertainment’.

Da Rest alisema tayari amesajili msanii wa kwanza na atazindua kampuni hiyo, msanii wake na albamu yake ya kwanza kwa wakati mmoja.

Ni zaidi ya mwaka mmoja tangu Da Rest kuanza kufanya kazi kama mwanamuziki huru baada ya kuondoka kwenye kundi la muziki la Juda Muzik.

Tangu wakati huo amezindua nyimbo kadhaa ukiwemo ‘Impore’ ambao amemhusisha DJ Pius.

Da Rest anasema wazo la kuanzisha kampuni lilichochewa na hitaji la kusaidia wasanii wanaoibuka pamoja na usaidizi aliopata wakati akianza na wala sio pesa.

Anapanga kusajili wasanii wawili zaidi kwenye Eeey D Entertainment, na atawafichua wakati mwafaka hasa baada yao kupita kiwango cha majaribio.

Share This Article