Coventry achaguliwa Rais wa kwanza mwanamke na Mwafrika wa kwanza IOC

Coventry ndiye mwanamke wa kwanza na pia Mwafrika wa kwanza, kuchaguliwa kuongoza IOC, na atahudumu kwa miaka minane.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kirsty Coventry kutoka Zimbabwe amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki – IOC –  kumrithi Thomas Bach anayestaafu.

Coventry, ambaye ni Waziri wa Michezo wa Zimbabwe, amezoa kura 49 katika kikao cha 144 cha IOC kilichokamilika leo Alhamisi nchini Ugiriki na kuwa Rais wa kumi wa kamati hiyo.

Juan Antonio Samaranch alimaliza wa pili kwa kura 28, akifuatwa na Rais wa Shirikisho la Riadha Ulimwenguni Lord Sebastien Coe kwa kura 8.

David Larpattient na Morinari Watanabe, walipata kura 4 kila mmoja huku Prince Feisal Al Hussein na Jonah Eliasch wakipata kura 2 kila mmoja.

Coventry ndiye mwanamke wa kwanza na pia Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa kuongoza IOC na atahudumu kwa miaka minane.

Website |  + posts
Share This Article