Susan Nakhumicha ashusha pumzi

Martin Mwanje
1 Min Read
Susan Nakhumicha - Waziri wa zamani wa Afya

Ni afueni kwa Waziri wa zamani wa Afya Susan Nakhumicha baada ya kuambulia uteuzi katika mabadiliko ya hivi punde yaliyofanywa serikalini. 

Rais William Ruto amemteua Nakhumicha kuwa Mwakilishi wa Kudumu katika Misheni ya Kudumu ya Kenya katika shirika la UN Habitat jijini Nairobi.

Tangu kufurushwa kwake serikalini, Nakhumicha amenukuliwa akilalamikia namna hali ilivyokuwa ngumu kwake hasa baada ya kushushwa cheo kutoka Waziri hadi raia wa kawaida.

Wakati mmoja, alinukuliwa akisema siku hizi yeye hujishughulisha tu na ukulima.

Nakhumicha aliondolewa kwenye wadhifa huo kuafuatia mabadiliko yaliyofanywa na Rais Ruto kufuatia maandamano ya vijana wa Gen Z yaliyorindima nchini mwezi Juni mwaka jana.

Wadhifa wake ulikabidhiwa Dkt. Deborah Barasa wakati milango ya upweke ikimlaki Nakhumicha baada ya kuondoka serikalini.

Website |  + posts
Share This Article