Chepkoech ashinda London Diamond League

Dismas Otuke
1 Min Read

Chepkoech ashinda mitaa 3000 kuruka viunzi na maji mashindano ya London Diamond League yaliyoandaliwa Uingereza Jumapili jioni.

Bingwa wa jumuiya ya madola Jackiline Chepkoech ameshinda mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji katika mkondo wa London Diamond League Jumapili jioni.

Chepkoech amesajili rekodi ya mkondo huo na pia muda wa kasi zaidi wa dakika 8 sekunde 57 nukta 55, akifautwa na Beatrice Chepkoech kwa dakika 9 sekunde 4 nukta 34.

Beatrice Chebet amemaliza wa pili katika mita 5,000 nyuma ya Gudaf Tsegay wa Ethioipia.

Tsgey ametumia dakika 14 sekunde 12 nukta 29 akifuatwa na Chebet kwa dakika 14 sekunde 12 nukta 92.

Mkondo huo wa 10 ndio wa mwisho kabla ya mashindano ya riadha ulimwenguni yatakayoandaliwa kati ya Agosti 19 na 27 mjini Budapest Hungary.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *