Chama cha wahariri wa habari chalaani mashambulizi dhidi ya wanahabari

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa chama cha wahariri wa habari Zubeida Kananu.

Chama cha wahariri wa habari nchini KEG, kimekashifu mashambulizi dhidi ya wanahabari wakati wa maandamano ya kupinga serikali.

Kupitia kwa taarifa iliyotolewa na rais wa chama hicho Zubeida Kananu, chama hicho kililalamika kuwa maafisa wa polisi walimpiga risasi na kumjeruhi Catherine Wanjeri Kariuki, ambaye ni mwanahabari wa kampuni ya Mediamax alipokuwa akitangaza wakati wa maandamano dhidi ya serikali katika mji wa Nakuru.

Kariuki alipata majeraha ya risasi kwenye paja na alikuwa akipokea matibabu Jumanne jioni.

Aidha chama hicho pia kilidokeza kuwa, maafisa wa polisi walimrushia mwanahabari wa shirika la CNN kemikali alipokuwa akifanya kazi katikati ya jiji la Nairobi.

Katika taarifa hiyo, chama hicho kililalamikia kile ilichokitaja utumizi mbaya wa risasi na vifaa vingine dhidi ya wanahabari pamoja na waandamanaji ambao hawana silaha.

“Kila mtu ana haki ya kushiriki maandamano ya amani na kuwasilisha malalamishi kwa serikali,” kilisema chama hicho huki kikinukuu sehemu ya 37 ya katiba.

Kilitoa wito wa kufanywa uchunguzi wa haraka wa shambulizi dhidi ya Kariuki and Muhire, kikitoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua za kisheria dhidi ya maafisa wa polisi waliohusika.

Website |  + posts
Share This Article