Kipute cha kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, kitaingia hatua ya robo fainali kesho nchini Misri.
Mabingwa mara saba Nigeria watakumbana na mabingwa watetezi Senegal kuanzia saa tisa, kabla ya wenyeji kupimana nguvu na Ghana saa kumi na mbili huku Morocco wakiwa na miadi dhidi ya Sierra Leone.
Afrika Kusini watamaliza udhia na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo saa tatu usiku.
Timu zitakazofuzu kwa nusu fainali zitawakilisha Afrika kwenye fainali za Kombe la dunia nchini Chile kati ya Septemba na Oktoba mwaka huu.