Tanzania ilitoa matokeo ya kushangaza zaidi ilipofuzu kwa nusu fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika,AFCON kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 nchini Morocco.
Tanzania walijikatia tiketi katika hatua ya nne bora, baada ya kuwagutusha Algeria, walipowanyuka mabao 4-3, kupitia mikiki ya penati.
Timu hizo zilikuwa zimetoka sare ya mabao 3-3 katika muda wa kawaida.
Tanzania sasa watakumbana na Misri katika nusu fainali Alhamisi hii.
Misri ilifuzu kufuatia ushindi wa magoli 4-1, dhidi ya Coted’ivore, katika robo fainali.
Wenyeji Morocco waliwatema nje Cameroon, bao moja kwa nunge katika hatua ya nane bora na wameweka miadi dhidi ya Senegal, katika nusu fainali ya kukata na shoka.
Senegal waliingia nusu fainali kufuatia ushindi wa amabo 4-2, kupitia changamoto ya penati baada ya kutoshana nguvu 1-1 ndani ya dakika 90.
Washindi wa nusu fainali watamenyana kwenye fainali Juni 2, huku washinde wakikutana katika mechi ya kuwania nishani ya shaba Juni mosi.
Mechi za nusu fainali
Mei 28 May, 2026
Egypt v Tanzania
Venue: Moulay El Hassan Stadium, Rabat
Senegal v Morocco
Venue: Moulay El Hassan Stadium, Rabat